BEKI wa kati wa Chelsea, David Luiz, amesema ameamua
kubaki katika klabu yake ya sasa kwa kukataa ofa ya Barcelona licha ya
kutangaziwa dau nono.
Beki huyowa kimataifa wa Brazil alikuwa katika rada
za Barca kutokana na timu hiyo kutaka kuimarisha safu yao ya ulinzi, lakini
alisisitiza kuwa ana majukumu ya kuifanyia miamba hiyo ya Stamford Bridge chini
ya Jose Mourinho.Akizngumza na gazeti la michezo la Brazil, Gazeta Esportiva, Luiz alisema: "Kulikuwa na ofa maalumu [kutoka Barcelona], lakini niliamua kwa makusudi kubaki Chelsea.
"Nina furaha kucheza katika klabu kubwa na kuwa katika kikosi cha timu ya taifa kwa ajili ya kuliwakilisha taifa langu."
Barcelona ilidaiwa kutangaza dau la pauni milioni 21.5 kwa ajili ya kumsajili Luiz Agosti mwaka huu, kiasi ambacho kilikuwa ni kidogo kwa Chelsea kushawishika kumuachia mchezaji huyo mwenye miaka 26.
Barca walikuwa wakimtaka Luiz kama mbadala wa beki
wa Paris Saint-Germain, Thiago Silva, ama beki wa Liverpool, Daniel Agger,
lakini walishindwa kuwasajili wote.
Majaaliwa ya kurudi uwanjani kwa Nahodha wa Barca, Carles Puyol yamekuwa shakani na kuamua kutaka kusajili mchezaji mwingine, kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Michezo wa Barca, Andoni Zubizaretta.
0 comments