NAHODHA wa timu ya Manchester City, Vincent Kompany anatarajia
kurudi uwanjani leo katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Viktoria
Plzen baada ya kuwa majeruhi toa kuanza kwa msimu huu.
Beki huyo wa kati mwenye umri wa miaka 27, alikuwa
nje ya uwanja baada ya kuumia nyonga katika mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa
Ligi Kuu ya England na timu yake imeshinda mchezo mmoja kati ya mitatu
waliyocheza bila nyota huyo.
Kocha Mkuu wa Manchester City, Manuel Pellegrini amesema
kuwa nyota huyo wa Ubelgiji kwa sasa yupo fiti japokuwa hakucheza katika mchezo
wa timu yake ya taifa dhidi ya Jamhuri ya Czech.
"Vincent amefanya mazpoezi na sisi kwa siku
mbili zilizopita," alisema Pellegrini. "Tutaangalia kama atakuwa fiti
kwa asilimia 100. Kama atakuwa fiti atacheza leo. Tutazungumza na daktari wa
timu na kutoa maamuzi.
"Nadhani yupo fiti kwa asilimia 100, lakini
kama itakuwa toifauti hatutamtumia. Tunakabiliwa na mchezo mgumu na muhimu sana
kweli lakini tutawatumia wachezaji wengine kama yeye hatakuwa fiti."
0 comments