BAADA ya mashabiki na uongozi wa klabu ya Manchester
United kuchomwa na mkuki wa moyo kutokana na taarifa za mshambuliaji wao wa
zamani Cristiano Ronaldo kusaini mkataba mpya wa Real Madrid, nyota huyo
amewatonesha jearaha hilo.
Staa huyo wa Ureno aliyekuwa akihusishwa na madai ya
kurudi katika klabu yake ya zamani, jana asubuhi aliongeza mkataba wa miaka
mitatu utakaofikia kikomo 2018 wa kuichezea Madrid na kuwa mchezaji anayelipwa
zaidi katika Ligi Kuu ya Hispania.
Ronaldo hadi sasa ameshaifungia timu yake ya Madrid
mabao 203 tangu alipotua klabuni hapo, amesema hana mpango wa kurudi tena
katika klabu yake ya zamani kwani ile itabaki kuwa historia tu, sasa yeye ni
mchezaji wa Madrid.
"Niwe mkweli kwako. Kila mtu anajua kuwa
nilikuwa Manchester kwa miaka sita, na walinipa vitu vingi na siwezi kusahau
hilo," alisema Ronaldo.
"Lakini Manchester imepita, sasa ni Madrid. Hana
ni nyumbani kwangu, familia yangu ipo hapa. Nina furaha sana kuwa hapa.
"Ninaiheshimu klabu yoyote ambayo inagonga hodi
na kuniulizia kuhusu mimi, lakini wanatakiwa kujua kuwa mipango yangu kwa sasa
ni kubaki hapa na kuichezea klabu hii labda hadi mwisho wa maisha yangu ya
soka.”
0 comments