MKURUGENZI wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), Sunday Kayuni atashiriki warsha ya wakufunzi wa makocha wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) itakayofanyika kuanzia Oktoba 22-24
mwaka huu.
Warsha hiyo iliyoandaliwa na CAF kwa ajili ya
wakufunzi wake itafanyika nchini Cameroon. Wakufunzi 18 wa CAF kwa upande wa
makocha watahudhuria warsha hiyo.
Madhumuni ya warsha hiyo ni kuainisha majukumu yao,
kubadilishana uzoefu. Pia kuwapa methodolojia mpya ya ufundishaji na muongozo
kuhusu mfumo wa leseni za makocha ambao watautumia katika nchi wanazotoka.
Mbali ya Kayuni Tanzania, wakufunzi wengine ni Ahmed
Babiker (Sudan), Amadou Shaibu (Nigeria), Boy Bizzah Mkhonta (Swaziland), Duodu
Fred Osam (Ghana), Edussei Anthony (Ghana), Fathi Nossir (Misri), Faouzy
Altaisha (Sudan) na Fran Hilton Smith (Afrika Kusini).
0 comments