WASANII wa Hip Hop Tanzania na nje ya Tanzania
wanatarajiwa kupanda jukwaa moja katika tamasha la Tanzania Hip Hop Music
Festival litakalofanyika kwenye Ukumbi wa New Msasani Club.
Tamasha hilo ambalo lililoandaliwa na Kundi la
Kikosi cha Mizinga linatarajiwa kufanyika Septemba 20 mwaka huu likiwa na lengo
la kuwakutanisha wasanii wa muziki huo wa Hip Hop wa ndani na nje ya nchi.
Akizungumza na Nyumba ya Michezo na Burudani,
kiongozi wa kundi hilo, Kalapina alisema tamasha hilo litakutanisha wasanii
kutoka katika nchi mbalimbali kwa lengo la kubadiliashana ujuzi ikiwa na pamoja
na kufikisha ujumbe wao kwa jamii kwa ujumla.
Kalapina aliwataja wasanii ambao watakaotumbuiza ni pamoja
na Cashmere kutoka New York, Marekani, Kimya wa Kenya wakati wasanii wa
nyumbani watakaopanda jukwaani ni LWP, Manzese Crew, Mchizi Mox, Big Dog PoseSerious
Manizzle, Viraka, Montel Foster na Kikosi cha Mizinga.
Kiongozi huyo alisema mbali na wasanii hao
kushambulia jukwaa lakini pia kutakuwa na mashindani ya freestyle pamoja na
kucheza brake dance, kiingilio katika tamasha hilo kitakuwa sh. 50,000 na
milango itakuwa wazi kuanzia saa 10 jioni.
0 comments