HATUA ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (Uefa)
inaendelea tena leo baada ya kumaliza michezo ya jana ambapo miamba 16 itashuka
uwanjani kuwania nafasi ya kutinga hatua ya 16 bora.
Atletico Madrid imekuwa katika mafanikio makubwa
Hispania na Ulaya watapata zawadi yao ya kwanza leo kama watashinda dhidi ya
Austria Vienna jijini Madrid na kufanikiwa kufuzu kwa hatua ya 16 bora ya Ligi
ya Mabingwa.
Vumbi jingine litatimuka kwa kuwashusha vinara wa
England, Arsenal na mahasimu wake Chelsea wakionyesha kazi na miamba ya
Bundesliga, Borussia Dortmund na Schalke 04.
Chelsea v Schalke 04
Chelsea wataikaribisha Schalke siku chache baada ya
kupokea kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Newcastle, kipigo hicho kilimfanya
Kocha Jose Mourinho kudai alifanya makosa
11. “Tupo katika nafasi nzuri ya kusonga mbele, lakini kama tutafungwa
tena basi tutajiweka kwenye hali ngumu,” alitadharisha Mourinho.
Basel v Steaua Bucharest
Basel wanawakaribisha Bucharest wakiwa na rekodi
mbaya ya kutoka sare kwenye mchezo wa kwanza hivyo sasa wanapigana kuhakikisha
wanapata tiketi ya kucheza Europa Ligi.
Borussia
Dortmund v Arsenal
Dortmund iliiharibu sherehe ya kuzaliwa Arsene
Wenger alipokuwa akitimiza miaka 64, waliposhinda 2-1 kwenye Uwanja wa
Emirates. Dortmund wanakwenda kwenye mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya ushindi
katika Bundesliga walipoichakaza Vfb Stuttgart
6-1. Arsenal wenyewe walishinda 2-0 dhidi ya Liverpool.
Napoli
v Marseille
Rafael Benitez ameiongoza Napoli kushinda mechi tatu
mfululizo za Serie A, na leo atakuwa mwenyeji wa Marseille ambao aliwafunga 2-1
kwenye mchezo uliopita. Matokeo hayo yameifanya timu hiyo ya Italia kuwa na
matumaini ya kufuzu kwa mtoano, akiwa sawa kwa pointi sita na Dortmund na
Arsenal, huku Marseille wakiwa hawana pointi yoyote.
Zenit
St Petersburg v FC Porto
Zenit wataiacha zaidi Porto katika harakati za
kusaka kufuzu kama watashinda leo na kufanya tofauti kati yao kuwa pointi nne
ikiwa wamekiza mechi mbili. Zenit walifanya kazi ya ziada kuwafunga Porto
kwenye mchezo uliopita walikutana hivyo kuifanya mechi ya leo kuwa na utamu wa
aina yake.
Atletico
Madrid v Austria Vienna
Atletico imetumia vizuri udhaifu wa kundi na
kujiweka katika nafasi nzuri ya kucheza 16 bora kwa mara ya kwanza tangu msimu
wa 2008/09. Pia ushindi wa Atletico utawafanya waweke rekodi ya kushinda mechi
nne mfululizo za michuano hiyo mikubwa ya Ulaya, wakivunja rekodi yao ya
kushinda mechi tatu msimu wa1958/59.
Ajax v Celtic
Ajax inahitaji japo pointi moja ili kujiweka katika
matumaini hata ya kupata nafasi ya tatu ya kucheza Europa Ligi. Celtic wenyewe
watakuwa wakisaka ushindi mwingine dhidi ya Wadachi hao ili kufufua matumaini
ya kucheza hatua ya mtoano kwa mara ya pili mfululizo.
Barcelona v AC Milan
Barcelona bado haijawa katika kiwango chake cha juu,
lakini inayo nafasi ya kucheza hatua ya 16 bora wakati watakapowavaa wachovu AC
Milan wanaondamwa majeruhi.
Shaka ya Barcelona ni ndogo kulianganisha na Milan
ambao wameanza msimu wa Serie A vibaya zaidi baada ya miaka 20 kupitia. Kama
Milan watafungwa na Barcelona na Celtic watashinda basi nafasi yao ya kusonga
mbele itakuwa finyu zaidi.
0 comments