Open top menu
Jumamosi, 2 Novemba 2013

TIMU za Azam FC na Mbeya City zimerudi kwenye nafasi zao za juu baada ya leo kushinda mechi zao za Ligi Kuu Tanzania Bara zilizochezwa kwenye viwanja vya Sokoine na Chamanzi.

Azam FC wameishusha Yanga kileleni baada ya kuitandika Ruvu Shooting mabao 3-0 na kufikisha pointi 26 ya kuwapiku mabingwa watetezi wa ligi hiyo kwa pointi moja.


Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mikubwa, mabao ya Azam yalifungwa na Kipre Tchetche dakika ya kwanza ya mchezo huo kabla ya Joseph Kimwaga kushindilia msumari wa pili dakika ya 45 na Khamis Mcha alimalizia bao la mwisho dakika ya 70.


Mbeya City nao wamerudi katika nafasi yake ya pili baada ya kuinyuka Ashanti United kwa bao 1-0 katika
mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.


Bao la kujifunga la Samir Ruhava dakika ya 38 liliisaidia Mbeya City kufikisha pointi 26 sawa na Azam FC
lakini wakizidiwa uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa.


Katika mchezo mwingine uliochezwa leo, Mtibwa Sugar waliitumia vizuri uwanja wa nyumbani baada ya
kuifunga Rhino Rangers bao 1-0, bao lililofungwa na Salim Mbonde dakika ya 44.


Mgambo Shooting waligawana pointi na Coastal Union baada ya kutoka suluhu katika mchezo wao
uliochezwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.


Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments