LIGI ya Mabingwa Ulaya inatarajia kuendelea tena leo
na kesho katika viwanja mbalimbali, lakini leo miamba 16 itashika uwanjani
kuwania pointi tatu ili kujiweka vizuri katika nafasi ya kucheza hatua ya
mtoano wa michuano hiyo mikubwa barani Ulaya.
Katika michezo hiyo nane lakini mechi ambazo
zinatarajia kuteka hisia za mashabiki wa soka duniani kote ni mchezo wa
mabingwa watetezi Bayern Munich pamoja na mabingwa wa zamani Real Madrid na
Manchester United.
Hapa chini ni michezo hiyo itakavyokuwa kwa kifupi
Real Sociedad v Man Utd
United watajihakikishia kucheza 16 bora kama
watapata ushindi Hispania baada ya kushinda mchezo wa kwanza 1-0 nyumbani kwao
dhidi ya Sociedad, ambayo inacheza kwa mara ya kwanza michuano hiyo baada ya
miaka 10. Manchester inaongoza kundi
hilo kwa pointi saba baada ya mechi tatu.
Sociedad imefunga bao moja katika mechi tatu za Ligi
ya Mabingwa hadi sasa na haina pointi yoyote, lakini ushindi wake wa mabao 5-0
iliyopata dhidi ya Osasuna ni ishara njema kabla ya mchezo wa leo.
Shakhtar v Bayer Leverkusen
Timu zote mbili zimefungwa katika ligi za kwao wiki
hii, Shakhtar wamenyukwa 2-0 na Volyn Lutsk, kikiwa ni kipigo cha tatu
mfululizo kwao, huku Leverkusen wakinyukwa1-0 na timu ya mkiani Eintracht
Braunschweig.
Leverkusen ilishinda katika mchezo wa kwanza walipokutana
Shakhtar mwezi uliopita, ushindi huo umewafanya kufikisha pointi sita, moja
nyuma ya vinara Manchester United.
Juventus v Real Madrid
Real Madrid imekusanya pointi tisa katika michezo
mitatu baada ya Cristiano Ronaldo kufunga mabao mawili wakishinda 2-1 dhidi ya
Juventus walipokutana mara ya mwisho na sasa wanahitaji sare tu kutoka kwa timu
hiyo ya Turin kujihakikishia kufuzu kwa16 bora.
Copenhagen v Galatasaray
Galatasaray ilishinda mechi ya kwanza kwa mabao 3-1
mjini Istanbul na kupanda hadi nafasi ya pili wakiwa nyuma kwa pointi tano kwa
Real, lakini mbili zaidi ya Juve na tatu kwa Copenhagen.
PSG v Anderlecht
Mabingwa wa Ufaransa wamefuzu kwa hatua ya mtoano
kwa mwaka wa pili mfululizo baada ya kuichakaza Anderlecht kwa mabao 5-0 katika
mchezo uliopita na kuweka rekodi ya kushindi mechi zote tatu katika kundi hilo.
Manchester City v CSKA Moscow
City iliweka kado ubaya wa hali ya hewa na
kufanikiwa kuifunga CSKA wiki mbili zilizopita katika mchezo ulioharibika kwa
kashfa ya ubaguzi wa rangi.
Ushindi dhidi ya miamba hiyo ya Russia
utawahakikisha kufuzu kwa hatua ya mtoano kwa mara ya kwanza baada ya kushindwa
kufanya hivyo mara mbili chini ya Roberto Mancini.
Viktoria Pilsen v Bayern Munich
Mabingwa watetezi wamethibisha kuwa hawafungiki kama
PSG, walithibisha hilo Jumamosi waliposhinda 2-1 dhidi ya Hoffenheim na kuweka
rekodi ya kutofungwa katikaBundesliga na kuifikia rekodi ya Hamburg iliyoweka
kati Januari 1982 na Januari 1983 waliposhinda mechi 36.
0 comments