Open top menu
Alhamisi, 7 Novemba 2013

JANA timu za England, Arsenal na Chelsea zilifanikiwa kuibuka na ushindi dhidi ya timu za Ujerumani, Borussia Dortmund na Schalke 04 katika Ligi ya Mabingwa ya Ulaya katika michezo ya hatua ya makundi.

Bao pekee la Aaron Ramsey dakika ya 62, limeipa Arsenal ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya wenyeji Dortmund nchini Ujerumani.

Hilo linakuwa bao la 13 kwa mchezaji huyo msimu huu na bao la tano katika michuano ya Ulaya msimu huu. Pamoja na kufungwa, wenyeji ndio waliocheza vyema usiku huu na kabla ya Arsenal kupata bao lake, hawakuweza kutengeneza nafasi hata moja ya kufunga. 

Borussia ambayo inapewa sifa ya moja ya timu bora kabisa Ulaya kwa sasa, iliingia kwenye mechi hiyo ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa 6-1 dhidi ya Stuttgart katika ligi ya kwao, Bundesliga, lakini ilikalishwa na mtutu mmoja wa bunduki.

Nayo Chelsea ambao walikuwa nyumbani kwenye Uwanja wa Stanford Bridge walifanikiwa kuibanjua Schalke kwa mabao 3-0 na kuongeza matumaini ya kutinga hatua ya mtoano wa michuano hiyo. 

Mabao mawili ya Samuel Eto'o dakika ya 31 na 54 na Demba Ba dakika ya 83 yalitosha kuipa ushindi vijana hao wa Jose Mourinho.

Katika mechi nyingine, Barcelona imeifunga AC Milan mabao 3-1 Uwanja wa Camp Nou, Lionel Messi akifunga mawili dakika ya 30 na 83, wakati lingine limefungwa na Busquets dakika ya 40, huku Pique akijifunga dakika ya 45 kuwapatia wageni bao la kufutia machozi.









Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments