MANCHESTER United imefanya mauaji makubwa ugenini,
baada ya kuitandika Bayer Leverkursen mabao 5-0 nchini Ujerumani katika mchezo
wa Ligi ya Mabingwa ya Ulaya.
Mabao ya United yamefungwa na Valencia dakika ya 22,
Spahic aliyejifunga dakika ya 30, Evans dakika ya 65, Smalling dakika ya 77 na
Nani dakika 88. Wayne Rooney ndiye alikuwa nyota wa mchezo kutoka na kupika
mabao manne katika ushindi huo ambao haukutarajiwa.
Katika mchezo mwingine, winga Gareth Bale
amewaongoza wachezaji 10 wa Real Madrid kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi
ya timu ya Roberto Mancini, Galatasaray, akifunga bao tamu la mpira wa adhabu
kipindi cha kwanza.
Huku Cristiano Ronaldo akiushuhudia mchezo huo
kutoka jukwaa la VIP Uwanja wa Bernabeu, hakuna aliyeweza kumzuia Bale kufunga
kwa mpira wa adhabu dakika ya 37.
Mabao mengine ya Real yalifungwa na Arbeloa dakika
ya 51, Di Maria dakika ya 63 Isco dakika ya 80, wakati bao pekee la Galatasaray
lilifungwa na Bulut dakika ya 38.
Manchester City nao wameifumua mabao 4-2 Viktoria
Plzen Uwanja wa Etihad katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya. Mabao ya City
yamefungwa na Aguero kwa penalti dakika ya 33, Nasri dkika ya 65, Negredo
dakika ya 79 na Dzeko dakika ya 90, wakati mabao ya Viktoria Plzen yamefungwa
na Horava dakika ya 43 na Tecl dakika ya 69.
Jana usiku mabingwa watetezi, Bayern Munich
wameendeleza ubabe katika Ligi ya Mabingwa baada ya kuicharaza mabao 3-1 CSKA
Moscow Uwanja wa Khimki Arena katika mchezo wa Kundi D.
Mabao ya Bayern usiku huu yamefungwa na Arjen
Robben, Mario Gotze na Thomas Muller kwa penalti. Huo unakuwa ushindi wa 10
mfululizo kwa Bayern na hivyo kuvunja rekodi ya mwaka 2002 ya Barcelona katika
michuano hiyo.
Winga wa Manchester United, Luis Nani akifunga bao la tano
Kiungo wa Real Madrid, Sergio Ramos akitolewa kwa kadi nyekundu
Mshambuliaji wa Galatasaray, Bulut akifunga bao pekee kwa timu yao
Mshambuliaji wa Manchester City, Aguero akishangilia bao
0 comments