SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemteua
Lina Kessy kuwa kamishna wa mechi ya Kombe la Dunia Kanda ya Afrika kwa
wanawake chini ya umri wa miaka 20 kati ya Afrika Kusini na Botswana.
Mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya kwanza
itachezwa nchini Afrika Kusini, Novemba 9 mwaka huu. Waamuzi kutoka Zambia
ndiyo watakaochezesha mechi hiyo namba kumi.
Waamuzi hao wataongozwa na Glads lengwe
atakayepuliza filimbi wakati mwamuzi msaidizi namba moja ni Bernadette Kwimbira
kutoka Malawi, namba mbili ni Mercy Zulu na mezani atakuwepo Sarah Ramadhani,
wote wa Zambia.
Afrika Kusini ilishinda mechi ya kwanza ugenini
mabao 5-2. Mshindi wa mechi hiyo atacheza raundi ya pili na mshindi wa mechi
kati ya Tanzania na Msumbiji.
Wakati huo huo, timu ya Taifa ya wanawake chini ya
miaka 20 (Tanzanite) kimewasili salama jijini Maputo, Msumbiji tayari kwa mechi
ya marudiano ya raundi ya kwanza ya Kombe la Dunia itakayochezwa kesho (Novemba
9 mwaka huu).
Kwa mujibu wa kiongozi wa msafara wa Tanzanite,
Kidao Wilfred ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF), timu hiyo chini ya Kocha wake Rogasian Kaijage
ilifanya mazoezi yake ya kwanza jana asubuhi.
Tanzanite itafanya mazoezi yake ya mwisho leo
(Novemba 8 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa wa Zimpeto ambao ndiyo
utakaotumika kwa mechi hiyo itakayochezwa kuanzia saa 10 kamili jioni kwa saa
za Msumbiji.
Nao wachezaji waliobaki kumalizia mtihani yao ya
kidato cha nne wameondoka leo saa 11 jioni kwa ndege ya LAM wakiongozwa na
naibu kiongozi wa msafara, Khadija Abdallah Nuhu ambaye ni mjumbe wa Kamati ya
Utendaji ya Chama cha Soka cha Zanzibar (ZFA).
0 comments