VIJANA wa Arsene Wenger wanaedhamilia kumaliza kiu
ya mataji kwa Arsenal baada ya jana kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa
Ligi Kuu England wakiwa na tofauti na pointi tano na anayemfuata.
Arsenal wamefikia pointi 25 wakiwa kileleni baada ya
jana kuitandika Liverpool mabao 2-0 wakifuatiwa na Chelsea wenye pointi 20 katika
msimamo huo sawa na Liverpool waliokuwa nafasi ya tatu.
Katika mchezo huo ambao ulikuywa na ushindani mkali
lakini Arsenal walionekana kutawala mchezo huo kwa muda mrefu, walipata bao la
kwanza kupitia kwa Santi Cazorla dakika ya 19 wakati bao la pili lilifungwa na
Aaron Ramsey dakika 59.
Matokeo hayo yanaweza kuwapa nguvu Arsenal ambao
wanasafiri kwenda Ujerumani kuvaana na Borussia Dortmund katika mchezo wa Ligi
ya Mabingwa Ulaya utakaochezwa Jumanne.
Mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney akifunga bao la tatu katika mchezo wa jana.
Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo, Manchester
United wameendelea kufufuka baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Fulham
United na kuwafanya kufikisha pointi 17 wakiwa katika nafasi ya nane katika
msimamo wa ligi hiyo.
Mabao ya United yamefungwa na Antonio Valencia,
Robin van Persie na Wayne Rooney na kuwafanya kuongeza matumaini ya kutetea
taji lao la ubingwa wa ligi hiyo.
Manchester City jana walivuna ushindi mnono wa mabao
7-0 dhidi ya Norwich City mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Etihad jijini
Manchester.
Pazia la mabao la City lilifungulia na bao la
kujifunga la Bradley Johnson wakati mengine yalifungwa na David Silva, Matija
Nastasic Alvaro Negredo, Yaya Toure, Sergio Aguero na Edin Dzeko alikamilisha
kalamu ya mabao katika mchezo huo.
Siku ya jana ilikuwa mbaya kwa Chelsea baada ya kukubali
kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Newcastle United, shukrani kwa mabao ya Yoan Gouffran na Loic Remy.
0 comments