BONDIA Mtanzania Omari Kimweri 'Lion Boy' anayefanya shughuli zake Deer
Park, Victoria, nchini Australia anatarajia kuwa mtanzania wa kwanza kupanda ulingoni Novemba 30, mwaka huu kugombea ubingwa wa Dunia unaotambuliwa
na WBC uzito wa kg 47.5.
Mpambano huo utakaopigwa nchini ya China na bingwa
wa dunia wa uzito huo nchini humo, Xiong Zhao Zhong ambaye ndiye anayeshikilia
taji hilo la ubingwa wa dunia WBC.
Kimweri anakuwa mtanzania wa kwanza kuwania taji
kubwa kabisa duniani akitokea nchini Austalia huku sapoti kubwa akitegemea
kutoka Tanzani ambapo alipozaliwa.
Kigezo cha kufanya apate pambano hilo kubwa ni
kutokana na rekodi yake pamoja na kutakiwa bondia mwenye asili ya Afrika ambapo
kula imemdondokea Kimweri kwa mara ya kwanza mtanzania huyo ataonekana Dunia
nzima akijaribu kuwania ubingwa wa WBC.
Kimweri kwa sasa yupo katika mazoezi ya mwisho ya
kujiandaa na mpambano huo amesema kuwa yeye binafsi yupo tayari kabisa kwa
mpambano huo, amewaomba Watanzania waendelee kumuombea kwani maombi hayo
yatamsaidia kunyakua taji hilo.
0 comments