Open top menu
Ijumaa, 15 Novemba 2013

TIMU ya taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ imepangwa kundi moja ya Mabingwa wa zamani wa Afrika, Zambia ambao ni timu mualikwa katika mashindano hayo ya Kombe la Chalenji inayotarajiwa kuanza Novemba 25 jijini Nairobi, Kenya.

Droo ya Chalenji iliyopangwa mapema leo jijini Nairobi, kutakuwa na makundi matatu ambapo kila kundi litatoa timu mbili kucheza hatua ya robo fainali ambazo zitaungana na timu mbili zenye matokeo mazuri kutoka katika makundi yote.

Kilimanjaro Stars wamepangwa kundi  B wakiwa na Zambia, Burundi na Somalia wakati kundi A kutakuwa na wenyeji Kenya, Ethiopia, Zanzibar na Sudani Kusini na kundi C linaundwa na mabingwa watetezi Uganda, Rwanda, Sudan na Eritrea.

Ratiba kamili ya michuano hiyo inatarajia kutolewa wiki ijayo na Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (Cecafa).


Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments