KITENDO cha Shirikisho la Mpira wa Miguu la
Kimataifa (Fifa) kutangaza kuongeza muda wa kupiga kura za kumchaguza mchezaji
bora wa dunia ‘Ballon d’Or 2013 kutoka Novemba 15 hadi Novemba 29 kimekuwa na
faida kubwa kwa Cristiano Ronaldo.
Maamuzi hayo yametafsiriwa ni kama ya kumbeba
Cristiano Ronaldo dhidi ya wapinzani wake kama Lionel Messi, Franck Ribery na
Zlatan Ibrahimovic, baada ya nahodha huyo wa Ureno kupiga hat trick dhidi ya
Sweden na kuipa tiketi timu yake ya Taifa kukata tiketi ya fainali za kombe la
dunia 2014.
Mwisho wa makocha, manahodha na waandishi wanaopiga
kura hizo kuwasilisha majina matatu ya juu ilikuwa November 15, saa kadhaa
baada ya kumalizika kwa michezo ya hatua ya mtoano na Rebery anayecheza Bayern
Munich alikuwa akipewa nafasi zaidi ya kuibuka na ushindi wa tuzo hiyo.
0 comments