KWA mara ya saba timu ya taifa ya kandanda ya
Cameroon imefaulu kuingia fainali za kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil
baada ya kuwachapa Tunisia 4-1 mjini Yaounde.
Mwezi uliopita wakati mataifa hayo mawili
yalipokutana katika uwanja wa Rades , nchini Tunisia matokeo yalikuwa suluhu ya
kutofungana bao lolote.
Lakini katika mechi iliyochezwa mjini Yaounde , siku
ya Jumapili jioni mshambuliaji Pierre Webo alifungua mvua ya mabao baada ya safu
ya ulinzi ya Tunisia kufanya masihara.
Na kabla ya kwenda mapumzikoni Benjamin Moukandjo
aliifungia Cameroon bao la pili kabla ya mchezaji wa akiba Ahmed Akaichi
kuipatia Tunisia bao lao moja na la pekee muda mfupi baadae.
Lakini kabla ya firimbi ya mwisho mchezaji Jean
Makoun aliiongezea Cameroon mabao mawili ya chap chap na kufanya matokeo kuwa
4-1 hivyo kuipa Cameroon tiketi ya kuwa timu mojawapo zitakazo wakilisha Afrika
katika kombe la dunia nchini Brazil mwaka 2014.
Awali ,timu za Ivory Coast na Nigeria zilikuwa
tayari zimejikatia tiketi ya kuwa wawakilishi wengine wa Afrika katika
mashindano hayo ya mwaka 2014.
0 comments