KOCHA Mkuu wa Kilimanjaro Stars, Kim Poulsen ametaja
kikosi cha wachezaji 23 watakaoshiriki michuano ya Kombe la Chalenji
inayofanyika nchini Kenya kuanzia Novemba 27 mwaka huu.
Kilimanjaro Stars iliyotwaa kombe hilo mara ya
mwisho mwaka 2010 chini ya Kocha Jan Poulsen, na ambayo imepangwa kundi B
katika michuano ya mwaka huu itacheza mechi yake ya kwanza Novemba 28 mwaka
dhidi ya Zambia kwenye Uwanja wa Machakos.
Wachezaji wanaounda kikosi hicho cha Tanzania Bara
ni makipa Deogratius Munishi (Yanga), Ivo Mapunda (Gor Mahia, Kenya) na Aishi
Manula (Azam). Mabeki ni Erasto Nyoni (Azam), Himid Mao (Azam), Ismail Gambo
(Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Michael Pius (Ruvu Shooting) na Said Moradi
(Azam).
Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga),
Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting),
Ramadhan Singano (Simba) na Salum Abubakar (Azam).
Safu ya ushambuliaji inaundwa na Elias Maguli (Ruvu
Shooting), Faridi Musa (Azam), Joseph Kimwaga (Azam), Juma Liuzio (Mtibwa
Sugar), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngasa (Yanga) na Thomas
Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).
Kilimanjaro Stars inatarajia kuondoka Jumatatu
(Novemba 25 mwaka huu) kwenda Nairobi kushiriki michuano hiyo itakayoanza
Novemba 27 mwaka huu na kumalizika Desemba 13 mwaka huu.
0 comments