TIMU ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ imeondoka
kuelekea nchini Kenya kwa mashindano ya kombe la chalenji linalotaraji kuanza
kuunguruma November 27.
Kilimanjaro Starz imeondoka na matumaini kibao ya
kurejea na kikombe hicho kutokana na maandalizi waliyoyafanya.
Wachezaji waliomo katika msafara huo ni makipa
Deogratius Munishi (Yanga), Ivo Mapunda (Gor Mahia, Kenya) na Aishi Manula
(Azam). Mabeki ni Erasto Nyoni (Azam), Himid Mao (Azam), Ismail Gambo (Azam),
Kelvin Yondani (Yanga), Michael Pius (Ruvu Shooting) na Said Moradi (Azam).
Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga),
Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting),
Ramadhan Singano (Simba) na Salum Abubakar (Azam).
Safu ya ushambuliaji inaundwa na Elias Maguli (Ruvu
Shooting), Faridi Musa (Azam), Joseph Kimwaga (Azam), Juma Liuzio (Mtibwa
Sugar), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngasa (Yanga) na Thomas
Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).
Hata hivyo, washambuliaji Samata na Ulimwengu
watajiunga na timu hiyo jijini Nairobi, Desemba Mosi mwaka huu wakitokea
Lubumbashi ambapo Novemba 30 mwaka huu TP Mazembe itacheza fainali ya Kombe la
Shirikisho Afrika.
Benchi la Ufundi la timu hiyo linawajumuisha Kim
Poulsen (Kocha Mkuu), Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha
wa Makipa), Leopold Tasso (Meneja wa Timu), Dk Mwanandi Mwankemwa (Daktari wa
Timu), Frank Mhonda (mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred Chimela (Mtunza Vifaa).
Kilimanjaro Stars ambayo ipo kundi B katika michuano
hiyo itacheza mechi yake ya kwanza Novemba 28 mwaka dhidi ya Zambia kwenye
Uwanja wa Machakos.
0 comments