WAAMUZI watatu wa Tanzania wameteuliwa na Baraza la
Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kuwa miongoni mwa waamuzi
18 watakaochezesha michuano hiyo huku Watanzania wakiwa wawili tu.
Michuano ya Cecafa mwaka huu imepangwa kuanza
kutimua vumbi kuanzia Novemba 27 mwaka huu jijini Nairobi, Kenya, Tanzania
itawakilishwa na waamuzi, Israel Mujuni mwamuzi wa kati na Fedinard Chacha mwamuzi
msaidizi wakati Waziri Sheha kutoka Zanzibar ni mwamuzi wa kati.
Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye alisema
waamuzi hao waliotangazwa wamegawanyika katika makundi mawili, nane ni waamuzi
wa kati wakati nane ni waamuzi wasaidizi.
Musonye alisema waamuzi hao wanatakiwa kufika Nairobi
kabla ya kuanza kwa michuano hiyo huku wakiwa wamejiandaa kwa kupimwa afya zao
pamoja na kuwa fiti.
Waamuzi wa kati waliokuwa katika orodha hiyo na nchi
zao kwenye mabano ni Anthony Okwayo (Kenya), Denis Batte (Uganda), Wish Yabarow
(Somalia), Louis Hakizimana (Rwanda), Thiery Nkurunziza (Burundi), Gebremichael
Luleseged (Eritrea) na Kheirala Murtaz (Sudan).
Waamuzi wasaidizi ni Gilbert Cheruiyot (Kenya), Tonny
Kidiya (Kenya), Mark Sonko (Uganda), Suleiman Bashir (Somalia), Fraser Zakara (Sudan
Kusini), Simba Honore (Rwanda), Hamid Idam (Sudan) na Kinfe Yimla (Ethiopia).
0 comments