SHIRIKISHO la Kimataifa la Mpira wa Miguu (Fifa)
imesema halina mpango wa kuhamisha michuano ya Fainali ya Kombe la Dunia 2014
kutoka nchini Brazil ingawa nchi hiyo imepata changamoto katika maandalizi ya
michuano hiyo.
Wafanyakazi wawili walipoteza maisha baada ya
kuangukiwa na nguzo ambazo ziliharibu uwanja wa Corithians ulio mjini Sao
Paulo.
Timu ya taifa ya Brazil inatarajiwa kucheza mechi ya
ufunguzi ya Kombe la dunia katika uwanja huo wenye uwezo wa kuwa na watazamaji
65,000.
Vyanzo vya habari vya juu ndani ya Shirikisho hilo
vimeendelea kusisitiza kuwa hakuna mbadala kutokana na kutokea kwa ajali hiyo.
Brazil ilikiri kuwa inafanya jitihada za kumaliza
ujenzi wa viwanja 12 kwa ajili ya michuano hiyo, sita kati ya hivyo ipo tayari
kwa ajili ya michuano ya kombe la shirikisho.
Ajali iliyotokea siku ya Jumatano ni ya tatu
kusababisha kifo katika viwanja vitakavyopigiwa kipute cha kombe la dunia. Wafanyakazi
wengine wawili walipoteza maisha kipindi cha miaka miwili iliyopita.
Uchunguzi umeanza hii leo kubaini chanzo cha ajali
mjini Sao Paulo.
0 comments