PICHA KWA HISANI YA BIN ZUBEIRY BLOG
ZANZIBAR Heroes imejiweka njia panda kwenda au kutokwenda
Robo Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Chalenji
baada ya kuchapwa mabao 3-1 na Ethiopia mchana wa leo, Uwanja wa Nyayo,
Nairobi, Kenya.
Mabao yaliyoizamisha Zanzibar leo yalifungwa na nahodha,
Fasika Asfan dakika ya tano, Salahadin Bargicho kwa penalti dakika ya 37 baada
ya Manaye Fantu kuangushwa kwenye eneo la hatari wakati Yonathan Kebede
alifunga la tatu dakika ya 83.
Bao la Zanzibar lilifungwa na kiungo mpya wa Simba
SC, Awadh Juma Issa dakika ya 68 kwa kichwa akiunganisha krosi ya Seif Abdallah
Karihe, ambaye alimlamba chenga beki wa kulia wa Ethiopia kwanza.
Zanzibar ilipata pigo mapema tu dakika ya 14, baada
ya mchezaji wake tegemeo Suleiman Kassim ‘Selembe’ kuumia nyama za paja na
kutoka nje, nafasi yake ikichukuliwa na Seif Abdallah Karihe.
Kwa kipigo cha leo, Zanzibar inabaki na pointi zake
tatu ilizovuna kwa kuifunga Sudan Kusini 2-1 katika mchezo wa ufunguzi na Ethiopia
iliyoanza kwa sare ya bila kufungana na wenyeji Kenya, inakuwa na pointi nne.
0 comments