Mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa akifunga bao la pili kwa kichwa katika mchezo wao dhidi ya JKT Ruvu. Yanga ilishinda mabao 4-0.
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanbga
leo imefanikiwa kukaa kileleni kwa mara kwanza tangu kuanza kwa msimu huu,
baada ya kuitandika bila huruma JKT Ruvu mabao 4-0 katika mchezo uliochezwa leo
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga ambao walianza ligi hiyo kwa kusuasua leo
wamefanikiwa kukaa kileleni baada ya kufikisha pointi 25 na kuwaacha Azam FC na
Mbeya City ambao walikuwa wanaongoza ligi hiyo wakiwa na pointi 23.
Azam na Mbeya City wanacheza leo na kama wakishinda
michezo yao wataishusha Yanga kileleni na kurudi wao huku idadi ya mabo nbdiyo
itakayoamua nani akae kileleni kati ya timu hiyo mbili.
Jerry Tegete akiwania mpira sambamba na beki wa JKT Ruvu, Nashon Naftar.
Mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa alifungua pazia
la mabao dakika ya nne ya mchezo huo
baada ya kufumua shuti kali nje ya eneo la 18 na kujaa wavuni huku kipa wa JKT,
Sadick Mecks ashindwe la kufanya.
Ngassa ambaye leo alikuwa mwiba kwa mabeki wa JKT,
alifunga bao la pili dakika ya 13 kwa kichwa akiunganisha mpira wa kurushwa wa Mbuyu
Twite na kutinga wavuni na kufanya timu yake iende mapumziko wakiwa mbele kwa
bao 2-0.
Mshambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbagu akimtoka beki wa JKT Ruvu, Damas Makwaya
Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko lakini
mabadiliko hayo yalikuwa na faida kwa upande wa Yanga kwani dakika ya 46 tu
walifanikiwa kupata bao la tatu lilifungwa na Oscar Joshua aliyeunganisha mpira
wa kona uliopigwa na Simon Msuva.
Mshambuliaji wa Yanga, Jerry Tegete alishindiliwa
msumari wa mwisho kwa JKT dakika 87 akimalizia kazi nzuri iliyofanywa na Msuva
na kuufanya ubao wa matokeo usomeka mabao 4-0.
Winga wa Yanga, Simon Msuva akimtoka beki wa JKT, Damas Makwaya
Mashabiki wa Yanga wakishangilia ushindi katika mchezo huo
Beki wa kushoto wa Yanga, Oscar Joshua akishangilia bao alilofunga katika mchezo huo
Mshambuliaji wa Yanga, Jerry Tegete akishangilia bao la nne alilofunga katika mchezo huo
Omary Mtaki akimdhibi Mrisho Ngassa asilete madhara langoni mwake
Omary Mtaki na Mrisho Ngassa wakiwania mpira
0 comments