ZANZIBAR imeanza vyema michuano ya Kombe la Mataifa
ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Chalenji baada ya kuifuga mabao 2-1 Sudan
Kusini katika mchezo wa ufunguzi wa Kundi A, Uwanja wa Nyayo, Nairobi, Kenya.
Mabao ya Zanzibar Heroes leo yalifungwa na kiungo wa
Coastal Union ya Tanga, Suleiman Kassim ‘Selembe’ dakika ya saba baada ya
kuipangua ngome ya Sudan Kusini na kufumua shuti lililomshinda kipa Juma Jinaro
na Adeyoum Saleh Ahmed dakika ya 67.
Bao la Sudan Kusini lilifungwa na Fabiano Lako
dakika ya 73, zikiwa ni dakika tano aiingie kuchukua nafasi ya Francis Khamis.
Zanzibar ingeweza kuondoka na ushindi mnene leo kama
washambuliaji wake, Khamis Mcha ‘Vialli’ na Ally Badru wangetumia vyema nafasi
nzuri walizopata.
Nafasi nzuri zaidi ambayo Zanzibar walipata ilikuwa
dakika ya 43 baada ya Badru kumlamba chenga kipa, lakini Khamis Mcha alipopiga mpira ukagonga mwamba na kipa akaudaka.
Zanzibar; Abdallah Rashid, Salum Khamis/Ally Khan
dk78, Waziri Salum, Shaffi Hassan, Mohamed Fakhi, Sabri Ali, Masoud Ali,
Suleiman Kassim, Awadh Juma na Khamis Mcha/Amour Omar dk44/Adeyoum Saleh dk62.
Sudan Kusini; Juma Jinaro, Atar Thomas, Philip
Delfino, Edomon Amadeo, Richard Justin, Wiiam Offiri, Jimmy Erasto, Thomas
Jacob, Godfrey Peter, Francis Khamis/Fabiano Lako dk68 na James Joseph.
0 comments