Open top menu
Jumapili, 10 Novemba 2013

YANGA tayari imemaliza na kipa mahiri, Juma Kaseja lakini atatambulia rasmi Novemba 15 baada ya dirisha dogoi la usajili wa wachezaji kwa msimu wa 2013/2014 Tanzania Bara litakapofunguliwa.

Dirisha hilo ambalo litatoa fulsa kwa klabu za ligi hiyo ambazo zimegundua mapungufu kwenye vikosi vyao hivyo kuamua kuongeza wachezaji wengine linatarajhiwa kufungwa rasmi Desemba 15 mwaka huu.

Kwa mujibu wa kanuni, klabu zenye fursa ya kusajili wachezaji katika dirisha dogo ni zile ambazo hazijatumia nafasi zote 30 za wachezaji.

Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) zimemaliza duru la kwanza msimu huu. Duru za pili litaanza kutimua vumbi Januari mwakani.

Kwa mujibu wa Kalenda ya Matukio ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) matukio ya Novemba na Desemba ni dirisha dogo la usajili na mechi za kirafiki za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)- FIFA Date.

Matukio mengine ni michuano ya Kombe la Uhai inayoshirikisha wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 wa klabu za VPL na michuano ya Kombe la Chalenji itakayofanyika Nairobi, Kenya.
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments