KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ameunda
kikosi cha wachezaji 32 kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya
Kenya (Harambee Stars) itakayochezwa Jumanne, Novemba 19 mwaka huu Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Kikosi hicho kinajumuisha wachezaji 16 walioitwa
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, na wengine 16 kutoka
Future Taifa Stars. Awali kambi ya Future Taifa Stars iliyoanza Novemba 9 mwaka
huu na kuvunjwa leo asubuhi ilikuwa na wachezaji 30.
Wachezaji walioitwa ni makipa wanne; Aishi Manula
(Azam), Ally Mustafa (Yanga), Deogratias Munishi (Yanga) na Ivo Mapunda (Gor
Mahia, Kenya). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Ismail Gambo (Azam), Kelvin
Yondani (Yanga), Michael Pius (Ruvu Shooting), Nadir Haroub (Yanga) na Said
Moradi (Azam).
Viungo wakabaji ni Erasto Nyoni (Azam), Himid Mao
(Azam), Shomari Kapombe (AC Cannes, Ufaransa) na Vincent Barnabas anayechezea
Mtibwa Sugar ya Morogoro.
Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga),
Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo, Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Jonas
Mkude (Simba), Ramadhan Singano (Simba), Salum Abubakar (Azam) na William
Lucian (Simba).
Viungo washambuliaji ni Faridi Musa (Azam), Joseph
Kimwaga (Azam), Mrisho Ngasa (Yanga), Mwingi Kazimoto (Markhiya, Qatar) na
Simon Msuva (Yanga).
Washambuliaji ni Elias Maguli (Ruvu Shooting), Juma
Liuzio (Mtibwa SugarMbwana Samata (TP Mazembe, DRC) na Thomas Ulimwengu (TP
Mazembe, DRC).
0 comments