MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Kagera
iliyochezwa jana (Oktoba 31 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza
sh. 32,726,000.
Washabiki waliohudhuria mechi hiyo namba 81
iliyomalizika kwa timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 walikuwa 5,541 ambapo
viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.
Mgawo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 4,992,101.69, gharama za kuchapa tiketi sh.
3,183,890 wakati kila klabu ilipata sh. 7,242,252.45.
Wamiliki wa uwanja walipata sh. 3,682,501.25,
gharama za mchezo sh. 2,209,500.75, Bodi ya Ligi sh. 2,209,500.75, Mfuko wa
Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,104,750.37, Chama cha Mpira wa Miguu
Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 859,250.29.
0 comments