Open top menu
Alhamisi, 29 Agosti 2013


Droo ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ‘Uefa’ imepangwa hivi karibuni na timu za Barcelona na Arsenal ndiyo timu ambazo zimepangwa kwenye makundi magumu kuliko miamba mingine ya soka barani Ulaya.

Katika droo hiyo Barcelona wamepangwa kundi H pamoja na AC Milan ya Italia, Ajax Amsterdam ya Uholanzi na Celtic ya Scotland ambapo katika kundi hilo timu mbili ndizo zinakazosonga mbele katika hatua ya 16 bora.

Kwa upande wa Arsenal na wenyewe watakuwa na kibarua kigumu katika hatua ya makundi ambapo wapo kwenye F wakiwa na Olympique Marseille ya Ufaransa, Borussia Dortmund ya Ujerumani na Napoli ya Italia.

Michezo ya msimu wa 59 ya michuano hiyo mikubwa barani Ulaya hatua ya makundi inatarajia kuanza Septemba 17, 2013 wakati fainali za michuano hiyo zinatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa da Luz uliopo jijini Lisbon, Ureno Mei 24, 2014.

MAKUNDI YA UEFA

Kundi A:
Manchester United, Shakthar, Leverkusen, Real Sociedad
Kundi B:
Real Madrid, Juventus, Galatasaray, FC Copenhagen
Kundi C:
Benfica, PSG, Olympiacos, Anderlecht
Kundi D:
Bayern Munich, CSKA Moscow, Man City, Viktoria Plzen
Kundi E:
Chelsea, Schalke, FC Basel, Steaua Bucuresti
Kundi F:
Arsenal, Marseille, Dortmund, Napoli
Kundi G:
FC Porto, Atletico Madrid, Zenit, Austria Vienna
Kundi H:
Barcelona, AC Milan, Ajax, Celtic
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments