ULIMWENGU wa soka una kiu ya kuona jinsi ya
wachezaji nyota duniani, Lionel Messi na Neymar watakapocheza pamoja katika
kikosi cha FC Barcelona msimu huu. Lakini pamoja na kuwepo kwa hamu hiyo pia
wachezaji hao kila mmoja atakuwa na cha kujifunza kitu kutoka kwa mwenzake.
Kwa kuwa Messi ni mchezaji bora wa dunia kwa sasa,
kuna uwezekano mkubwa wa Neymar kujifunza vitu vingi kutoka kwa nyota huyo kuhusu
soka na maisha kwa ujumla.
Angalia mambo saba ambayo Neymar atajifunza kutoka
kwa Messi na akiyafuata vizuri ni wazi kuwa Mbrazil huyo atakuja kuwa tegemeo
katika siku za usoni.
Jinsi
ya kudanganya
Messi na Neymar tayari wana vitu ambavyo vinafanana
vya kufanyiwa sana faulo na mabeki, lakini Messi ana uwezo mkubwa wa kutumia
ujanja wake kuwahadaa mabeki ili wamuangushe na kupata faulo ambazo mara nyingi
zinafaida kwa timu yake, Neymar ambaye silaha yake kubwa ni kujiangusha
anatakiwa kusoma ujanja huo wa Messi ambaye hutumia zaidi mguu wake wa kulia
kwa kuuacha nyuma na mabeki hujikwaa na kumuangusha.
Uvumilivu
Kutokana na uchanga wake katika soka, Neymar anatakiwa
kusoma somo la uvumilivu kutoka kwa Messi. Neymar anapokuwa na mpira huwa na
haraka ya kutaka kwenda mbele ili kufunga lakini kwa Messi huamini kwa kupiga
pasi huku wakitawala mpira na mwisho wake hupata goli ambalo hulitafuta kwa
mipango.
Umuhimu
wa kujituma
Wachezaji wa Barcelona huwa wanajituma kwa lengo la
kusaka ushindi na wanapoona mambo ynakuwa magumu hurudisha mpira nyuma kwa
Messi na kuanza mashambulizi upya kwa kuwa wanaamini kuwa anaweza kuumiliki
mpira, Neymar hana sifa hiyo ya kurudi nyuma na kuanza upya akifika eneo la
hatari, hicho anatakiwa kujifunza kwa Messi.
Kutengeneza
bao na kufunga vina muhimu sawa
Wachezaji hawa wawili wote ni mafundi kwa
kuzifumania nyavu duniani. Lakini unaweza kuwa mchezaji bora zaidi bila ya kufunga
mabao. Messi ana uwezo mkubwa wa kuwaunganisha wachezaji kwa kuwatengenezea
nafasi za kufunga kitu ambacho kimekosekana kwa Neymar na ili awe mchezaji bora
anatakiwa kujifunza hicho kwa Messi.
Uwiano
wa majivuno na unyenyekevu
Ili uwe mchezaji bora duniani unatakiwa kuwa na
uwiano wa majivuno na unyenyekevu, Neymar
ukiacha kupata mafanikio akiwa bado mchezaji mchanga lakini pia ndiyo umri wake
pia unakua, mtu sahihi wa kumwambia hiki hapana na hiki kizuri ni Messi kwa
kuwa amepitia katika hatua hizo.
Ushirikiano
Hili ni somo kubwa sana kwa Neymar kulisoma kutoka
kwa Messi kwani mshambuliaji huyo kwake mafanikio ya klabu ndiyo kitu muhimu
kuliko yake binafsi. Neymar anatakiwa kuiga mfano wa Messi kwa kuisaidia kwanza
Barcelona na mafanikio yake yatakuwa baadaye.
Jinsi
gani atakuwa bora
Kuna tofauti ya kuwa mshindi na kuwa mfalme. Messi
ni mmoja kati ya washindi katika soka kwa sasa, ameshinda tuzo nne ya uchezaji
bora duniani. Neymar ni mchezaji chipukizi mwenye mafanikio kwa sasa, anatakiwa
kujifunza kwa Messi anawezaje kuwa bora zaidi ya alivyosasa.
0 comments