Open top menu
Jumanne, 20 Agosti 2013



Beki wa Manchester City, Vicent Kompany


MANCHESTER, England
NAHODHA wa timu ya soka ya Manchester City, Vincent Kompany, huenda akawa
mashakani kucheza katika michezo ya hivi karibuni baada ya kujisikia maumivu mara
baada ya kumalizika klwa mchezo wa jana.

City ilifanikiwa kuichapa timu ngumu ya Newcastle United kwa mabao 4-0 jana usiku, na
nahodha wa wababe hao, akitarajiwa kuonana na madaktari mchana huu kwa ajili ya vipimo
zaidi.

Kwa mujibu wa taarifa hizo kutoka katika klabu ya mabingwa hao wa zamani wa Ligi Kuu
England, Kompany, maarufu kama 'Vinny', alianza kujisikia maumivu juu ya kinena.

Kocha wa City, Manuel Pellegrini, anaonekana kukosa uhakika kama mchezaji huyo
atamtua au la alipozungumza na waandishi mara baada ya mchezo wa jana usiku.

Maumivu ya kila mara ya Kompany yanaonekana kuwa ya kuzoeleka sasa, ambapo hata
mwaka jana beki huyo wa kimataifa wa Ubelgiji alikuwa katika wakati mgumu wa kumalizia
msimu vizuri, ambapo alikuwa akisumbuliwa na kifua mara kwa mara.
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments