Deco de Souza
KIUNGO wa zamani wa timu za Barcelona na Chelsea,
Deco, ametangaza rasmi kustaafu soka siku ya sherehe yake ya kuzaliwa kutimiza
miaka 36 mwaka huu.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno alianza soka yake
katika klabu ya Salgueiros nchini Brazil kabla ya kuhamia Porto 1999, na kuwa
raia wa nchi hiyo.
Kutokana na ushiriki wa klabu hiyo katika michuano
ya Ligi ya Mabingwa Ulaya 2004, aliondoka na kuhamia Primeira Liga akiichezea
Barcelona, akitumia miaka kwa miamba hiyo ya Camp Nou kabla ya kutua Stamford
Bridge kwa misimu miwili.
Aliondoka katika soka ya Ulaya akiwa bado na kiwango
kizuri 2010, na alirudi Brazil kwenda kuitumikia klabu ya Fluminense, na kuamua
kutundika daluga baada ya miaka mitatu akiwa na miamba hiyo ya Amerika Kusini.
"Kwa majonzi na masikitiko makubwa, natangaza
kuwa huu ndiyo mwisho wa kucheza soka ya kimataifa," alinukuliwa akisema
hivyo katika mtandao wa AS.
"Dakika ya mwisho nikiwa na Fluminense Jumatano
iliyopita ilikuwa ya mwisho katika uchezaji wa soka yangu ya kimataifa kwa
miaka 17 sasa.
"Ningependa kuendelea hadi mwisho wa Ligi Kuu
ya hapa (Brasileiro) na kuifanya timu yangu kurudi katika michuano ya
Libertadores, lakini mwili wangu hauwezi kuniruhusu.
"Nina furaha sana kwa kufikia mafanikio haya na
uaminifu wa mashabiki katika timu zote nilizowahi kuzitumikia."
Kiungo huyo mshambuliaji aliitumikia Ureno kwa
michezo 75 ndani ya miaka saba aliyopanza kuitumikia timu hiyo ya taifa,
akiiwakilisha timu katika michuano mikubwa miwili ya Kombe la Ulaya na miwili
ya Kombe la Dunia.
0 comments