MICHUANO
ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2013/2014 inaanza kutimua vumbi kesho
(Agosti 24 mwaka huu) katika viwanja saba tofauti huku mabingwa watetezi Yanga
wakianza kutetea ubingwa wao kwa kuikaribisha Ashanti United kwenye Uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam.
Uwanja
wa Manungu ulioko Turiani mkoani Morogoro utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya
Azam ya Dar es Salaam na wenyeji Mtibwa Sugar. Oljoro JKT itaikaribisha Coastal
Union kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha.
Mgambo
Shooting itaoneshana kazi na JKT Ruvu ambayo hivi sasa iko chini ya Kocha
Mbwana Makata. Mechi hiyo itachezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga wakati Rhino
Rangers itakwaruzana na Simba katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Mbeya
City iliyopanda VPL msimu huu itapimana ubavu na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa
Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya huku Ruvu Shooting ikiialika Mabatini,
Mlandizi timu ya Tanzania Prisons kutoka Mbeya.
0 comments