Open top menu
Jumanne, 20 Agosti 2013


Nahodha wa Manchester City, Vicent Company 'Vinny'

IMEFAHAMIKA muda huu kuwa Nahodha wa Manchester City, Vicent Kompany 'Vinny' atakuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki tatu hadi nne.

Uchunguzi uliokuwa ukifanyikwa kwa mchezaji huyo asubuhi ya leo umebaini kuwa ameumia juu ya kinena katika mchezo wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Newcastle uliopigwa jana usiku.

Hiyo ina maana kuwa Kocha wa City, Manuel Pellegrini, anatakiwa kutafuta mbadala wa beki huyo katika michezo yake mitatu migumu, ukiwamo ule dhidi ya mahasimu wao wa jiji moja, Man United.

Baada ya kuangalia jinsi alivyoumia katika mchezo wa jana usiku dhidi ya Newcastle, jopo la madaktari wa timu ya taifa ya Ubelgiji walimfanyia uchunguzi na kubaini kuwa hataweza kuwa uwanjani kwa kwa zaidi ya wiki tatu hadi nne.
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments