Open top menu
Jumanne, 20 Agosti 2013

Kocha wa Manchester United, David Moyes

MANCHESTER, Uingereza
KLABU ya Manchester United inaandaa ofa mpya ya pauni milioni 35 kwa ajili ya kurudi kwa Everton ikitaka kuwasajili beki Leighton Baines na kiungo mshambuliaji Marouane Fellaini.
Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England (Barclays Premier League), awali walishuhudia ofa yao ya pauni milioni 28 ikikataliwa na Everton jana, na sasa wameonesha nia zaidi ya kuwataka wachezaji hao kwa kuongeza fedha.
Habari ambazo zimevuja muda si mrefu zinasema kuwa licha ya United kutaka kuwasajili wachezaji hao, miamba ya Merseyside imesisitiza kuwa haitaki kuwaachia, lakini Kocha wa United, David Moyes, ambaye aliondoka Goodison Park kujiunga na miamba ya Old Trafford katika majira ya joto mwaka huu, anajipanga kuwasajili wachezaji wake hao wa zamani.
Wakati hali ikiwa hivyo, Everton idaiwa kutaka kutaja dau la pauni milioni 40 kwa ajili ya kuwaachia wachezaji hao wawili, na United bado inahangaika kuona kama inaweza kuwasajili kabla ya siku ya mwisho ya usajili.
Hata hivyo, imefahamika kuwa pauni milioni 35 zinaweza kutolewa na United. Gawanyo lake ni kwamba pauni milioni 12 ni kwa ajili ya Baines na 23 kwa Fellaini.

Wachezaji wa Everton wanaotakiwa na Manchester United, Leighton Baines na Marouane Fellaini 
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments