Open top menu
Jumatano, 28 Agosti 2013



Kiungo wa Bayern, Bastian Schweinsteiger 




KIUNGO wa timu ya soka ya Bayern Munich, Bastian Schweinsteiger, anaweza kuukosa mchezo wa fainali ya Uefa Super Cup dhidi ya Chelsea baada ya kuumia kifundo cha mguu katika mechi ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Freiburg.

Schweinsteiger alilazimika kutolewa baada ya kucheza kwa dakika 10 wakati Bayern ikianza kwa kuongoza kwa bao lililofungwa Xherdan Shaqiri.

Lakini Freiburg walichomoa Nicolas Hofler dakika ya 88 na kukiacha kikosi cha kocha Pep Guardiola kukosa nafasi ya kujiongezea ponti tatu muhimu huku ikimkosa Schweinsteiger.

" Schweinsteiger ameumia kifundo cha mguu (ankle),” kocha huyo Mhispania alisema. “Atafanyiwa vipimo kesh. Nafikiri anaweza kucheza Ijumaa, lakini bado hatulijui hilo.

"Tulicheza vizuri. Lakini ukiwa unaongoza kwa 1-0 katika ligi ya Bundesliga, vitu kama hivi vinaweza kutokea. Hatukuacha kushambyulia na tulikuwa na nafasi kadhaa. Lakini najivunia sana kuwa na wachezaji kama hawa.”

Nahodha wa Bayern, Philipp Lahm alikubaliana na maoni ya kocha wake, akiamini kuwa yeye na wenzake wanapaswa kujilaumu wenyewe kwa kupata sare hiyo.

“Tujilaumu wenyewe,” Lahm aliuambia mtandao wa klabu yake (fcbayern.telekom.de). “Tuliruhusu bao la kusawazisha kabla ya mchezo kumalizika, lakini tulikuwa na nafasi ya kuongeza mabao zaidi kabla hata ya kusawazisha kwao.

“Kama tungekuwa na mabao zaidi isingekuwa hivi. Katika mechi chache zilizopita, tumeshindwa kupata matokeo kwa tatizo kama hili, na huwa tunaadhibiwa kwa hilo.”
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments