Mshambuliaji Robin van Persie leo ametangazwa kuwa
mchezaji bora wa timu hiyo kwa mwezi wa Agosti wa Manchester United, ikiwa ni
tuzo yake ya kwanza tangu alipotua katika klabu hiyo akitokea Arsenal.
Straika huyo wa kimataifa wa Uholanzi amefanikiwa
kutawazwa kuwa mchezaji bora wa mwezi baada ya kupata 57% ya kura zilizopigwa
wakati Nemanja Vidic alipata 26% na aliyeshika nafasi ya tatu ni Danny Welbeck alipata
17%.
Van Persie ambaye ameichezea Manchester United
michezo 50 ya mashindano yaote tangu atue klabuni hapo, ametwaa tuzo hiyo baada
ya kufanikiwa kufunga mabao manne katika michezo mitatu aliyocheza mwezi huu.
“Siku zote kushinda tuzo ni jambo zuri sana, hasa
unapopigiwa kura na mashabiki,” alisema Vana Persie.
0 comments