Kocha wa PSV Eindhoven, Phillip Cocu
KOCHA wa timu ya soka ya PSV Eindhoven, Phillip Cocu,
amesema timu yake imejiandaa kwa lolote wakati timu yake ikijiandaa kuivaa AC
Milan kwa ajili ya mchezo wa marudianbo wa kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
PSV na Milan wanakutana katika Uwanja wa San Siro
leo baada ya kwenda sare ya bao 1-1 Jumatano iliyopita, ambapo miamba hiyo ya
Uholanzi ililazimika kusawazisha bao waliloruhusu mapema kwenye mchezo huo.
Na wakati miamba hiyo ya Italia ikihitaji hata
suluhu kuweza kufuzu na kuingia katika hatua ya makundi, Cocu ana uhakika kuwa
timu yake inaweza kuibuka na ushindi wa ugenini.
“Kucheza nyumbani ni tofauti na unapokuwa ugenini,”
alianza kwa kusema Cocu. “Tulicheza mchezo mzuri tulipokuwa Eindhoven na nina
uhakika kuwa tutacheza vizuri pia leo katika mchezo wetu wa mjini Milan.
“Ni wakati mzuri kwangu na pamoja na timu kwa ujumla,
nah ii inakuja pale ambapo tunaona tunaweza kushindana na timu ngumu kama Milan.
“Hii inaleta wasiwasi mkubwa wakati mwingine, lakini
ni wasiwasi chanya, ni kitu ambacho unahitaji kuwanacho katika soka. Kazi yangu
pia ni kusaidia wachezaji kupata uzoefu huu na kukabiliana na presha.
“Tumejiandaa kwa kila kitu. Sijui Milan watakuja na
mbinu gani, kama watazuia ama watashambulia. Kwa mchezo kama huu muhimu, chochote
kinaweza kutokea katika makosa madogo.”
Milan itakuwa ikimkaribisha tena kiungo wa kimataifa
wa Brazil, Robinho na beki kinda, Mattia De Sciglio, baada ya wachezaji hao
kuwa fiti kwa ajili ya mchezo huo.
Hata hivyo, Cocu bado hana matumaini licha ya Milan
kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Hellas Verona katika mchezo wa Ligi Kuu ya Italia ‘Serie
A.
“Milan ina uwezo mkubwa wa kuchagua aina ya
wachezaji wazuri wa kuwatumia,” Cocu alisema. “Tunatakiwa kuingia uwanjani
tukijua kabisa kuwa tuna wajibu wa kuwazuia wachezaji hawa.”
0 comments