Open top menu
Jumatano, 28 Agosti 2013


Klabu ya Chelsea imemgeukia mshambuliaji wa Anzhi Makhachkala, Samuel Eto’o baada ya kushindwa kumng’oa straika wa Manchester United, Wayne Rooney ambaye klabu yake imegoma kumuuza kwa mahasimu wao hao.

Klabu hiyo yenye maskani yake jijini London ipo katika mazungumzo na mwakilishi wa mchezaji huyo ambaye tayari amekubali makubaliano ya awali ambnapo Chelsea nimepanga kumpa mkataba wa miaka miwili.

Eto'o tayari ameonyesha nia ya kuhamia Chelsea lakini dili hilo linapata nguvu zaidi baada ya Jose Mourinho ambaye tayari ana washambuliaji wanne lakini hadi sasa hakuna aliyeifungia bao timu hiyo, washambuliaji hao ni Fernando Torres, Romelu Lukaku na Demba Ba.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa kimataifa mwenye miaka 32, anatarajiwa kusaini mkataba katika klabu hiyo kwa ada ya uhamisho ya paundi 1.7 milioni. Mpango huo unaweza kukamilika kwa haraka kutokana na klabu ya Anzhi Makhachkala kupunguza gharama kwa mchezaji huyo.

Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments