Open top menu
Jumamosi, 24 Agosti 2013

  Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Linah pichani kati akiwa na madensa wake wakitumbuiza jukwaani usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 ndani ya uwanja wa Al-Hassan Mwinyi. Tamasha hilo linaandaliwa na kampuni bingwa ya Burudani hapa nchini,Prime Time Promotions Ltd kwa kushirikiana na Clouds FM,na kudhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake murua kabisa cha Serengeti Premium Lager.
 Anaitwa Amin,mmoja wa wasanii mahiri akiwaimbisha mashabiki wake usiku huu kwenye u kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,linalofanyika kwenye uwanja wa Al-Hassan Mwinyi. 
 Wenyewe mashabiki waki wanamuita Baba Levo na yeye kabaki Levo kwenye gemu ya muziki wa bongofleva,ndiye pichani Baba Levo akiwaimbisha mashabiki wake kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 ndani ya uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani Tabora.
 Wanamuita Mzee wa Masauti,Christian Bella akiwaimbisha mashabiki wake wa muziki wa dansi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta,liinalofanyika usiku huu kwenye uwanja wa Al-Hassan Mwinyi.
 Wakali wa kudansi kutoka THT,wakijulikana kwa jina la Makomanda wakionesha umahiri wao wa kucheza jukwaani usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013.
 Mmoja wakali wa hip hop, Stamina akikamua jukwaani vilivyo usiku huu mbele ya umati wa wakazi wa mji wa Tabora na vitongoji vyake waliojitokeza kushuhudia makamuzi ya wasanii mbalimbali wa tamasha la Serengeti Fiesta 2013.
 Msanii machachari wa muziki wa bongofleva/filamu Shilole akiimba huku akiwa amebebwa na shabiki wake,huku shangwe na miluzi za mashabiki zikiwa zimetawala kila kona.
 Anajiita Raisi wa Manzese, kutoka  kundi la Tip Top Connections,atambulikae kwa jina la Madee akiwaimbisha mashabiki wake wimbo wake wa NANI KAIBA POMBE YANGU,usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013.
 Msanii wa muziki wa bongofleva,Rachael akicheza jukwaani na mmoja wa madensa wake,huku mashabiki wake wakipiga mayowe ya shangwa kuonesha kukunwa vilivyo na msanii huyo.
 Sehemu ya  umati wa mji wa Tabora waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,linalofanyika kwenye uwanja wa Al-Hassan Mwinyi.
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments