Open top menu
Ijumaa, 23 Agosti 2013






Mashabiki wa timu ya Simba wakifuatilia moja ya mechi za timu yao katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

TIMU ya soka ya Rhino Rangers imechimba mkwara mzito juu ya mashabiki watakaojitokeza kwa ajili ya kuangalia tamasha kubwa la muziki la FIESTA katika Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi usiku wa leo.
Mkwara huo umetokana na kutokuwa na imani na watu ambao watakuwa katika uwanja huo utakaotumika katika mchezo wa kwanza wa timu hiyo dhidi ya Simba SC.
Uongozi wa Rhino, ambayo inamilikiwa na Jeshi, hautaki kuona uwanjani hapo (pitch), ili uwanja huo uweze kuwa salama kwa ajili ya mchezo wao wa kesho, ambapo wanaiogopa Simba wakidai inaweza kuweka vitu vyenye imani ya kishirikina.
Nyumba ya Michezo na Burudani lilidokezwa kuwa hali hiyo imetokana na maafande hao kuwaogopa Simba katika Nyanja ya ufundi nje ya uwanja, ambapo wamejipanga kuanza kwa ushindi wa nyumbani.

"Hali kwa sasa iko hivyo hapa, na mashabiki wote ambao watajitokeza katika tamasha la Fiesta wameshawekewa maonyo uwanja mzima kuwa hawatatakiwa kugusa eneo la kuchezea mpira, na maafande wenyewe wameimarisha ulinzi," alisema mwandishi wetu wa Tabora.

Wakati hali ikiwa hivyo mkoani Tabora, Uwanja wa Taifa hali ni shwari, ambapo mabingwa watetezi, Yanga watakuwa na kazi ngumu mbele ya vijana waliopanda kwa mara nyingine katika ngazi ya Ligi Kuu, Ashanti United.

Endelea kutembelea katika mtandao wako wa Nyumba ya Michezo na Burudani kwa mambo mengi zaidi kuhusu Ligi Ku na Burudani kwa ujumla.
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments