Open top menu
Jumatano, 21 Agosti 2013



Klabu ya Real Madrid itashuka uwanjani kwa miezi mitatu bila ya kuwa na kiungo wake mkongwe, Xabi Alonso ambaye amevunjika mfupa katika mguu wake wa kulia.

Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo, imesema kiungo huyo baada ya kufanyiwa uchunguzi amegundulika amevunjika mfupa wa juu wa juu wa mguu wake wa kulia hivyo atakuwa nje ya uwanjani kwa miezi mitatu.

Nyota huyo ana uwiano wa kucheza michezo 40 katika mashindano yote inayoshiriki Madrid kwa msimu, aliumia katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi ya Hispania, La Liga dhidi ya Real Betis ambao walishinda mabao 2-1 mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo Alonso anatarajiwa kurudi uwanjani mwishoni mwa mwezi Novemba au mwanzoni mwa Desemba kama atafanyiwa uchunguzi na kuhakikisha kuwa mguu wake umepona vizuri.
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments