Open top menu
Jumanne, 20 Agosti 2013





PAMOJA na aliyekuwa kipa wa Simba, Juma Kaseja kutokuwa na timu baada ya kuachwa na timu yake ya zamani lakini Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen amemjuisha katika kikosi chake kitakachoivaa Gambia katika mchezo wa mchujo ya Kombe la Dunia utakaochezwa Septemba 7 mwaka huu nchini humo.
                                             
Kaseja alitemwa mwishoni mwa msimu ulioipita kwa madai ya kushuka kwa viwango ameitwa katika timu ya wachezaji 24 wanaotarajiwa kuingia kambini Agosti 29 mwaka huu kabla ya saa 1 kamili usiku. Kambi ya Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itakuwa kwenye hoteli ya Accommondia jijini Dar es Salaam.

Mbali na Kaseja wachezajki wengine walioitwa katika kikosi hicho ni pamoja na makipa Mwadini Ali (Azam), Ally Mustafa (Yanga) na Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Shomari Kapombe (Simba), Nadir Haroub (Yanga), Erasto Nyoni (Azam), Vincent Barnabas (Mtibwa Sugar) na David Luhende (Yanga).

Viungo Khamis Mcha (Azam), Salum Abubakar (Azam), Said Dilunga (Ruvu Shooting), Frank Domayo (Yanga), Athuman Idd (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Amir Kiemba (Simba), Mrisho Ngasa (Yanga), Simon Msuva (Yanga), John Boko (Azam), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo) na Juma Liuzio (Mtibwa Sugar).
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments