Open top menu
Jumatatu, 26 Agosti 2013


 Saa nne usiku leo dunia itasimama kupisha mchezo wa kukata na shoka kati ya Chelsea itakuvaana na Manchester United kwenye Uwanja wan Old Trafford.

Mchezo huo leo umebeba vitu vingi ambavyo vimeufanya uonekane kuwa na mvuto wa aina yake na kuvuta hisia za mashabiki lukuki wa soka duniani kote.

Kivutio cha kwanza katika mchezo huo ni pale timu hizo ziotakapovaana zikiwa na makocha wawili wapya ambao watakuwa katika benchi kwa mara ya kwanza miamba hiyo itakapokutana.

Jose Mourinho atakuwa anaiongoza kwa mara ya pili ataivaa Manchester United wakati kwa upande wa David Moyes atakuwa kwenye benchi la Man Utd akivaana na Chelsea.

Utamu mwingine katika mchezo huo utakuwa pale mshambuliaji wa Manchester United, wayne Rooney anayewania kwa hali na mali na Mourinho, ataanza katika kikosi cha kwanza cha United.

Mashabiki wa soka duniani kote wana kiu ya kujua kama nyota huyo ambaye Mourinho anamsubiri mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo atafanya nini atakapokuwa uwanjani leo?

Leo hakuna mtu atakayetumwa dukani wakati miamba hiyo iutakapokuwa uwanjani kusaka pointi tatu muhimu katika msimamo wa Ligi Kuu ya England.

DONDOO MUHIMU

Timu: Manchester United v Chelsea
Uwanja: Old Trafford
Muda: Saa 4:00 Usiku
Mfumo: Manchester United 4-4-1-1
              Chelsea FC 4-4-1-1

Vikosi: Manchester United: De Gea, Jones, Ferdinand, Vidic, Evra,     
             Valencia, Carrick, Giggs, Cleverley, Welbeck, Van Persie.
             Chelsea: Cech, Ivanovic, Terry, Cahill, Cole, Hazard, Lampard,  
             Ramires, Mata, Oscar, Lukaku.
Mwamuzi: Martin Atkinson

Fuatana nasi baadaye upate kila kitakachotea wakati wa mchezo huo  

Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments