Open top menu
Alhamisi, 22 Agosti 2013

Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi



KLABU ya soka ya Barcelona inasubiri ripoti ya madaktari kuona kama mshambuliaji wao, Lionel Messi, ambaye anahofiwa kuwa atakuwa na tatizo katika misuli ya paja baada ya kulazimika kutolewa wakati wa mapumziko katika mchezo wa sare ya bao 1-1 dhidi ya Atletico Madrid.

Bao la kwanza kwa Neymar akiwa Camp Nou lilizima lile walilofungwa mapema na mshambuliaji wao wa zamani, David Villa, ukiwa ni mchezo wa kwanza wa michuano ya Super Cup uliopigwa jana usiku, lakini kutolewa kwa Messi kuliwafanya wageni kupata nguvu zaidi.


"Messi alilazimika kutolewa baada ya kulalamikia misuli ya paja lake la kushoto," ilisomeka taarifa iliyokuwa katika mtandao wa klabu hiyo wakati mchezo ukikaribia kumalizika.


Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Argentina anatarajiwa kufanyiwa vipimo leo mchana ili kupata majibu ya tatizo lake, huku akiacha wasiwasi kwa timu yake kama tatizo alilopata linafanana na lile lililomfanya kushindwa kumaliza msimu uliopita vizuri.

Messi alipata maumivu kama hayo katika mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Paris Saint-Germain.

Na mchezo uliofuata aliingia akitokea benchi na kuisaidia Barca kupata ushindi, lakini nyota huyo mwenye miaka 26 aliumia tena na kuacha michezo mitatu ya mwisho ya La Liga wakati timu yake ikiwa tayari imetwaa ubingwa.
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments