Open top menu
Jumatano, 28 Agosti 2013


Kikosi cha Yanga




MICHUANO ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inaingia raundi ya pili leo kwa timu zote 14 kuwa katika viwanja tofauti.


Lakini pambano linaloonekana kuvuta hisia za watu ni lile kati ya timu ya Yanga dhidi ya Coastal Union ya Tanga.

Mechi hiyo inapigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10.30 jioni, ambapo kiingilio kwa mujibu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ni sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000. Mwamuzi aliyepangwa kuchezesha mchezo huo ni Martin Saanya kutoka Morogoro, wakati Kamishna ni Omari Walii wa Arusha.

Mechi nyingine itakuwa katika Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro, ambapo Mtibwa Sugar inaikaribisha Kagera Sugar, wakati katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora, wenyeji Rhino Rangers Rangers watakuwa wakiialika Azam FC ya Dar es Salaam.

Vumbi lingine litatimka kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi, Pwani, wakati maafande wa JKT Ruvu watakapokwaruzana na wenzao wa Tanzania Prisons kutoka Mbeya. Mbeya City na Ruvu Shooting zitacheza kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Jiji la Tanga litakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Mgambo Shooting na Ashanti United itakayochezwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani. Oljoro JKT itakuwa mwenyeji wa mabingwa wa zamani, Simba kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha.
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments