Open top menu
Jumatano, 28 Agosti 2013


Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga jana walibanwa mbavu baada ya kulazimishwa sare na Coastal Union baada ya mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam kumalizika kwa sare 1-1.

Mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa sana kuanzia dakika ya kwanza hadi mwisho hali iliyosababishwa kutawaliwa na kadi nyingi za njano sambamba na nyekundu.

Yanga ndiyo walikuwa wa kwanza kuandika bao la kuongoza dakika ya 69 lililofungwa na Didier Kavumbagu akimalizia krosi safi iliyopigwa na David Luhende ambaye alichachafya ngome ya Coastal Union.

Coastal iliwalazimu wasubiri hadi dakika ya majeruhi ndiyo wapate bao la kusawazisha lililofungwa na Jerry Santo kwa njia ya penalti baada ya kushika mpira akiwa eneo la hatari na mwamuzi wa mchezo huo, Martine Saanya kuamuru adhabu hiyo.

Mchezo huo ambao uliatawaliwa na vurugu za hapa na pale hali iliyosababisha wachezaji wengi waonywe kwa kadi ya za njano na nyekundu na Saanya.

Saanya katika mchezo huo alityoa kadi 10 za njano na mbili nyekundu, wachezaji waliotolewa kwa nkadi nyekundu ni Crispine Odula na Simon Msuva ambao waligombana uwanjani, wakati wlaioonywa kwa kjadi ya njano ni Juma Nyosso, Didier Kavumbagu, Haruna Moshi 'Boban', Salum Telela, Simon Msuva mbili, Suleiman Kassim 'Solembe', Husein Javu, Yayo Lutimba na Haruna Niyonzima.

Baada ya mchezo huo Kocha wa timu ya Coastal, Hemed Moroco alisema ameridhika na kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wake lakini mwamuzi alivuruga mchezo huo lakini kwa kuwa mwamuzi ni binadamu hana matatizo naye.

Kwa upande wake Kocha wa Yanga, Ernie Brandts alisema mchezaji bora katika mchezo huo alikuwa mwamuzi, kwani alivuruga sana mchezo huo na matokeo hayo yametokana na kile alichokitaka mwamuzi.

Matokeo ya michezo yote iliyochezwa leo ni kama ifuatavyo

Simba 1-0 JKT Oljoro
JKT 3-0 Prisons
Ruvu Shooting 1-2 Mbeya City
Mgambo 1-0 Ashanti United
Mtibwa 1-0 Kagera
Azam 2-0 Rhino
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments