Yohan Cabaye akiwa kazini
BAADA ya kuangukia pua katika mchezo wa kwanza wa
Ligi Kuu ya England, klabu ya Arsenal imetenga kitita cha pauni 10 milioni
(zaidi ya 22 bilioni) kusana saini ya kiungo wa Newcastle, Yohan Cabaye.
Arsenal ambayo inamwania Luis Suarez wa Liverpool,
ilianza vibaya msimu huu baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa
Aston Villa hali ambayo imeibua mjadala mkubwa kwa mashabiki wa klabu hiyo
ambao wapo waliomtaka kocha wake Arsene Wenger kuachia ngazi.
Cabaye,27, alisafiri na timu yake hadi Manchester
kuivaa Manchester City lakini hakucheza mchezo huo ambao waliambulia kipigo cha
mabao 4-0, lakini alirudi nyumbani akionyesha kuwa hayupo tayari kiakili
kuichezea timu hiyo kwa sasa.
"Sitaki
kuiamini ofa ya Arsenal," alisema Kocha wa Nerwcastle, Alan Pardew kuhusu
ofa ya Arsenal.
Cabaye ambaye ameichezea Newcastle michezo 73 hadi
sasa na kuifungia mabao 11 anatakiwa Arsenal kwa lengo la kuimarisha sehemu yao
ya kiungo baada ya wachezaji wake kuwa majeruhi kama Mikel Arteta na Abou
Diaby.
Newcastle hawana mpango wa kumuuza Cabaye, lakini
hawanashindwa kuamia kwa haraka ili wasije yakawakuta kama yaliyoptokea kwa
mshambuliaji wao, Andy Carroll mwaka 2011 ambaye walidai kuwa hawezi kuuzwa kwa
dau lolote lile lakini mwisho wake walimuuza kwa Liverpool kwa ada ya uhamisho
wa pauni 35 milioni.
0 comments