MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga imeanza vizuri mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo baada ya kuitandika bila huruma timu ya Ashanti United mabao 5-1 katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Wakati Yanga wakiikaribisha Ashanti kwa kipigo cha mbwa
mwjizi mahasimu wao Simba wamepanwa mbavu mjini kwenye Uwanja wa Ali Hassan
Mwinyi mjini Tabora na Rhino Rangers baada ya kutoka sare ya mabao 2-2.
Mabao ya Yanga katika mchezo huo yalifungwa na Jerry
Tegete dakika ya 11 na 47, Simon Msuva dakika ya 58, Haruna Niyonzima dakika ya
73 na Nizar Khalfan dakika ya 90 wakati bao la Ashanti lilifungwa na Abdallah
Juma dakika ya 87 ya mchezo huo.
Kwa matokeo hayo Yanga inaongoza ligi hiyo ikiwa na
pointi tatu na mabao matanonya kufungwa huku wakifungwa bao ikiwa ni mwanzo
mzuri wa kutetea ubingwa wao.
Michezo mingine ya ligi hiyo, Ruvu Shooting
waliibuka na ushindi mnono dhidi ya Prisons ya Mbeya wa mabao 3-0 katika mchezo
uliochezwa kwenye uwanja wa Mabatini Mlandizi.
Mtibwa ambao walikuwa wenyeji wa Azam FC katika
uwanja wa Manungu nje kidogo ya Morogoro walishindwa kuutumia vizuri uwanja wao
wa nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya mabao 1-1 na Wanarambaramba.
Coastal Union wameanza kwa kishindao ligi hiyo baada
ya kushinda mchezo wake wa ugenini mjini Arusha kwa kuitandika JKT Oljoro mabao
2-0 mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Kumbukumbu za Shekh Amri Abeid.
Mchezo mwingine Maafande wa JKT Ruvu walianza vizuri
ligi hiyo baada ya kuitandika wajeda wenzao Mgambo Shooting ya Tanga mabao 2-0
mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
Mbeya wakiwa katika uwanja wa nyumbani waliibana
mbavu Kagera Sugar na kuilazimisha sare ya bila kufungana katika mchezo mwao
uliochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Matokeo
ya mechi za leo
Yanga 5-1 Ashanti
Mtibwa 1-1 Azam
FC
JKT Oljoro 0-2
Coastal
Mgambo 0-2 JKT
Ruvu
Rhino 2-2 Simba SC
Mbeya City 0-0 Kagera
Ruvu 3-0 Prisons
0 comments