Open top menu
Alhamisi, 22 Agosti 2013


Ivanovic (kulia) akionekana kumpiga kiwiko Benteke


BEKI wa Chelsea, Branislav Ivanovic, amenusurika kuingia katika adhabu ya Chama cha Soka England (FA) licha ya kuonekana kumpiga kiwiko mshambuliaji wa Aston Villa, Christian Benteke, katika mchezo wa jana usiku.

Kocha wa Aston Villa, Paul Lambert, alikuwa mwenye hasira kwa mwamuzi wa mchezo huo, Kevin Friend, aliyeamua kutompa kadi nyekundu beki huyo wa kimataifa wa Serbia kwa tukio hilo, sekunde chache kabla ya kuifungia Chelsea bao la ushindi.

Lakini kwa sababu Friend alimuonesha kadi ya njano beki huyo, na aliliona tukio hilo la kupigwa kwa kiwiko Benteke, FA haitachukua hatua yoyote.

Sheria za FA zilibadilishwa katika majira ya joto kwa tukio kama hilo msimu uliopita, ambapo mchezaji wa Wigan, Callum McManaman, ambaye alikimbia adhabu kwa kumchezea vibaya mchezaji wa Newcastle, Massadio Haidara.

Hata hivyo, sheria hiyo inasema kuwa FA wangeweza kumchukulia hatua zaidi mchezaji huyo kama mwamuzi aneandikakatika ripoti yake kuwa hakuliona tukio hilo.
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments