Open top menu
Jumatano, 28 Agosti 2013


MCHEZO wa pili kwa timu za Yanga ya Dar es Salaam na Coastal Union ya Tanga.

Yanga inashuka uwanjani ikiwa na pointi tatu ikiongoza katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa ushindi wake wa mabao 5-1, wakati Coastal pia ikiwa na pointi tatu kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya JKT Oljoro.

Mchezo huu unatarajiwa kuwa mkali kutokana na timu zote mbili kufanya usajili wa nguvu, ambapo kuongezeka kwa Yayo Lutimba raia wa Uganda, Juma Nyosso na Haruna Moshi 'Boban' wote kutoka Simba na Uhuru Selemani aliyotoka Azam kunaifanya Coastal kuonekana timu yenye ushindani mkubwa msimu huu.

Ikiwa imemaliza katika nafasi ya sita msimu uliopita, Coastal imeanza kwa uhai zaidi msimu huu kwa ushindi wa ugenini Jumamosi iliyopita mkoani Arusha, wakati Yanga, ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu wanaotetea taji lao msimu huu wakianza kwa kuiangamiza bila huruma Ashanti United iliyopanda msimu huu.

Licha ya mchezo huu hapa Uwanja wa Taifa, timu nyingine 12 zinazofanya jumla ya timu 14 za Ligi Kuu zinashuka katika viwanja tofauti hapa nchini.

Endelea kubaki na Nyumba ya Michezo na Burudani upate kujua kinachoendelea katika uwanja huu ni viwanja vingine sita ambako michezo ya Ligi Kuu inaendelea.
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments