Open top menu
Jumanne, 20 Agosti 2013





LONDON, Uingereza
KIUNGO wa England, Scott Parker, amekubali kusaini mkataba wa miaka mitatu kukipiga katika timu ya Fulham, baada ya kukataa ofa ya kujiunga na kocha wake wa zamani, Harry Redknapp, katika klabu ya QPR.

Parker amefanya safari fupi katika jiji la London ili kujiunga na kikosi cha Kocha Martin Jol, na Fulham ni timu ya tano kwa mchezajihuyo kucheza nchini humo.

Parker alisema: "Nina furaha kujiunga na Fulham na nitafurahi sana kukutana na wachezaji wenzangu wapya katika mazoezi kesho asubuhi.

"Fulham ni timu iliyoendelea katika Ligi Kuu ya England 'Premier League' na najipanga kuisaidia zaidi katika maendeleo ya klabu kwa ujumla katika miaka mitatu nitakayokuwa hapa."

Kocha wa Fulham, Martin Jol, naye aliongeza: "NIna furaha kuona kwamba Scott amejiunga nasi. Ni kiungo ambaye hawezi kuchoka kirahisi kwa ajili ya timu yake na ni mchezaji mzuri akiwa na mpira na hata asipokuwanao.

"Inapendeza kuona mchezaji mwenye uwezo na heshima kama  yake kuichezea Fulham akiwa ameonesha ubora wake katika Ligi Kuu na timu ya taifa kwa miaka kadhaa. Nina furaha kwamba yuko hapa na ataanza mazoezi kwa ajili ya mchezo wetu ujao nyumbani.

Parker alianza soka ya kimataifa akiwa na klabu ya Charlton, kabla ya kujiunga na Chelsea. Baadaye alijiunga na Newcastle, lakini alirudi nyumbani akiwa na mafanikio na kujiunga na West Ham, ambapo alipata tuzo ya Mchezaji Bora wa wa Tuzo ya Waandishi wa Habari wa England.

Kushuka kwa United kutoka Ligi Kuu kulimpa njia ya kurudi Ligi Kuu tena, ambapo Parker alijiunga na Spurs, na alipokuwa na miamba hiyo ya White Hart Lane ndipo alipochaguliwa kuiongoza England katika mechi ya kimataifa ya kirafiki akiwa kama nahodha dhidi ya Uholanzi.

Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments